Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema kuwa bila kuangalia historia ya wapinzani wetu US Gandarmerie tutaingia Jumapili kwa lengo moja kupambana na kupata ushindi.
Ahmed amesema hatutawadharau Gandarmerie licha ya kuwa hawana uzoefu na historia kubwa kwenye michuano hii kama sisi lakini tutachukua tahadhari zote ili tusifanye makosa.
Ahmed ameongeza kuwa tuliwahi kufanya makosa zamani na kupoteza mechi dhidi ya UD Songo na Jwaneng Galaxy katika uwanja wa nyumbani hatua ambayo hatutaki ijirudie.
Kuhusu hali ya kikosi Ahmed amesema tutaendelea tutamkosa kiungo, Hassan Dilunga ambaye ni majeruhi wa muda mrefu lakini wengine wapo kamili na jana wamefanya mazoezi.
“Kwa sasa lengo letu ni kuingia robo fainali, tukilala tukiamka tunawaza hilo. Ukiangalia kwenye karatasi sisi ni bora zaidi ya Gandarmerie lakini hatutawachukulia poa bali tutaingia kwa tahadhari zote.
“Huko nyuma iliwahi kutokea mara mbili tukashindwa kufuzu tukiwa katika uwanja wa nyumbani lakini safari hii tumejipanga kuhakikisha hilo halitokei tena. Ndoto ya Wanasimba wote ni kutinga robo fainali,” amesema Ahmed.
2 Responses