Ahmed: Tukilitaka jambo letu hakuna wa kutuzuia

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amesema tumejiandaa ndani na nje ya uwanja kuelekea mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ahmed ameyasema hayo wakati wa kufungua zoezi la hamasa kuelekea mchezo huo katika Tawi la Tunawakera lililopo Keko Maduka Mawili.

Ahmed amesema hakuna jambo lolote litakalotuzuia kwenda robo fainali hata kama wataungana dunia nzima lakini Jwaneng Galaxy anakufa Jumamosi kwa Mkapa.

Ahmed ameongeza kuwa Jwaneng wamekuja wakati mbaya ambao tunahitaji kushinda na tunahitaji kwenda robo fainali kwahiyo hakuna chochote kitafanya tusitimize malengo yetu.

“Simba anapohitaji robo fainali hakuna timu yoyote ya kuzuia, hata waungane wote, sisi ndio wenye mashindano haya na tunajua njia ya kufuzu.

“Kufuzu robo fainali tunategemea Wanasimba wote, tukisimama kwa pamoja na kujitokeza kwa wingi Benjamin Mkapa Jwaneng Galaxy kitamkuta kama kilichomkuta Horoya,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER