Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema wapinzani wetu Power Dynamos kutoka Zambia wanatarajia kuwasili nchini kesho saa 12 jioni.
Ahmed amesema msafara wa Power Dynamos utawasili kwa Shirika la Ndege la ATCL na moja kwa moja utaelekea hotelini ambapo watafikia.
Ahmed amesema waamuzi pamoja na maafisa wa mchezo huo watawasili nchini Jumamosi, Septemba 30.
Akizungumzia hali ya kikosi Ahmed amesema, “timu ipo kwenye hali nzuri wachezaji wanaendelea na mazoezi chini ya kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’.
“Kuelekea mchezo wa Jumapili bado tutaendelea kuwakosa mlinda mlango Aishi Manula, mlinzi Henock Inonga na kiungo mshambuliaji Aubin Kramo ambao ni majeruhi,” amesema Ahmed.