Ahmed: Ni furaha kutwaa taji kwa kuifunga Yanga

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa hatuna nafasi ya kuchukua taji la Ligi Kuu msimu huu ndiyo maana tumeweka nguvu kubwa katika Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambayo Jumamosi tunacheza nusu fainali dhidi ya Yanga.

Ahmed amesema kuchukua taji la ASFC itakuwa faraja kubwa kwa Wanasimba lakini kuifunga Yanga Jumamosi itakuwa jambo bora litakalotufanya kumaliza msimu kwa furaha.

Ahmed ameongeza kuwa kikosi kinaendelea vizuri na mazoezi na wachezaji waliokuwa wamepata majeraha wanaendelea vizuri na tunategemea watakuwepo kwenye mchezo wa Jumamosi.

“Mlinda mlango Aishi Manula aliumia vidole viwili kabla ya mchezo wetu dhidi ya Geita Gold lakini anaendelea vizuri na anafanya mazoezi ya kucheza mpira na wachezaji wa ndani, na kwa matibabu anayopata tunatarajia atakuwa fiti kabla ya mchezo.

“Shomari Kapombe naye anaendelea vizuri pamoja na Clatous Chama ambaye alianza mazoezi mepesi Jumatatu na wote tunatarajia watakuwa tayari kwa mchezo wa Jumamosi,” amesema Ahmed.

Ahmed amewaomba pia mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya kuisapoti timu kuhakikisha tunaibuka na ushindi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER