Ahmed: Jumanne iwe mvua iwe jua ushindi lazima kwa Mkapa

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema hakuna jambo jingine tunalihitaji zaidi ya ushindi katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa Jumanne katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ahmed amesema ushindi dhidi ya Vipers utatuongezea nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali kwakuwa tutakuwa tumefikisha pointi sita.

Ahmed amesisitiza kuwa ushindi dhidi ya Vipers ni jukumu la Wanasimba wote kuanzia viongozi, benchi la fundi, wachezaji mpaka mashabiki na kila mmoja anapaswa kutimiza nafasi yake.

“Jumanne tuna jukumu zito Wanasimba, tunahitaji kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu. Ni matumaini yetu kila mmoja akitimiza jukumu lake Vipers hatoboi.

“Siku ya mchezo tumeteua jukwaa la chini ya TV kubwa pale kwa Mkapa, vikundi vyote vya hamasa vitakaa pale au yoyote anayejiweza hatuta pumzika dakika zote 90,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER