Ahmed: Hatukupewa nafasi ya kufungua AFL kwa bahati mbaya

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetupa uwenyeji wa kufungua michuano ya African Football League (AFL) kutokana na ubora pamoja na wingi wa mashabiki wetu.

Ahmed amesema CAF wanafahamu Simba ni miongoni mwa timu bora barani Afrika ndio maana wametupa nafasi hii na wanajua hatuwezi kuwaangusha.

Ahmed ameyasema hayo katika muendelezo wa hamasa kuelekea mchezo huo wa ufunguzi dhidi ya Al Ahly katika Viwanja vya Bakhersa vilivyopo Manzese, Dar es Salaam.

Ahmed ameendelea kuwasisitiza mashabiki wetu kutoka Manzese kuhakikisha wanakata tiketi mapema ili kuondoa usumbufu siku ya Ijumaa.

“Simba ni timu kubwa Afrika, CAF hawajafanya bahati mbaya kutupa uwenyeji wa kufungua michuano ya AFL kwakuwa wanajua tuna timu bora na mashabiki wengi pia.

“AFL ni michuano mikubwa na inashirikisha timu kubwa, mfano Simba isingekuwepo Tanzania basi kusingekuwa na timu ambayo ingewakilisha kutoka hapa nchini,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER