Ahmed: Hatujilaumu, bali tumejifunza

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema hatujilaumu kwa kutolewa na Al Ahly katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika bali tumejifunza ili wakati mwingine tukishiriki tuwe bora zaidi.

Ahmed amesema Al Ahly ndio Mabingwa watetezi wa michuano hii, ndio timu ya Karne ya Afrika na pia kinara wa kuchukua mara nyingi taji hili kwahiyo kutolewa nao sio jambo la kusema tutakaa na kuanza kujilaumu.

Ahmed ameongeza kuwa katika miaka sita tumeingia mara tano robo fainali na timu zote tulizocheza dhidi yao zimepotea lakini Simba imeendelea kubaki pale pale na sasa muda umefika wa kusonga mbele.

“Tulianza kucheza na TP Mazembe wakapoteza mpaka sasa ndio wanarejea, tukacheza na Kaizer Chiefs wao wamepoteza, ikaja Orlando Pirates na wamepoteza na msimu uliopita Wydad Casablanca nao wameishia hatua ya makundi lakini Simba iko vile vile kwahiyo sio jambo jepesi,” amesema Ahmed.

Ahmed ameongeza kuwa baada ya kurejea nyumbani tunaelekeza nguvu katika michuano ya Ligi pamoja na CRDB Bank Federation Cup.

“Kikosi kitaondoka kesho kuelekea Kigoma kwa ajili ya mchezo wetu wa hatua ya 16 bora dhidi ya Mashujaa FC utakaopigwa Jumanne saa 10 jioni Uwanja wa Lake Tanganyika na baadae tutaelekea Singida kucheza na Singida Black Stars,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER