Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amewaongoza Wanasimba kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Simba kuelekea kilele cha Simba Day.
Kila mwaka kuelekea Simba Day tunakuwa na shughuli mbalimbali za kijamii na zoezi la uchangiaji damu linakuwepo ndani yake.
Kwa upande wa hapa Dar es Salaam tulikuwa na vituo vitatu ambapo Ahmed amechangia damu katika Kituo cha Karume wakati Wanasimba wengine wakichangia Kituo cha Kariakoo Jengo la zamani.
Kituo kingine cha uchangiaji kulikuwa Buguruni Ofisi ya Mtendaji wa kata na Wanasimba wengi wamechangia.
Uongozi wa klabu unafahamu umuhimu wa damu kwakuwa tunajua kuna Watanzania wenzetu wengi wapo mahospitalini wakiwa na uhitaji na wanahitaji kupata msaada kutoka kwetu.