Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amewaongoza Wanasimba kuchangia damu ikiwa ni uzinduzi wa Wiki ya Simba.
Ahmed amechangia damu katika Kituo cha Karume wakati Wanasimba wengine wakichangia Kituo cha Chamazi.
Akizungumzia zoezi hilo wakati likiwa linaendelea, Ahmed amewaomba Wanasimba waendelee kuchangia damu katika maeneo waliopo ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji.
“Leo tumezindua wiki ya Simba na tumeanza kwa kuchangia damu hapa Karume wengine wanachangia Chamazi.
“Hii ni kwa Wanasimba wote nchi nzima, uhitaji wa damu ni wa kila mtu, leo sisi ni wazima kesho tunaweza kuwa wagonjwa tukahitaji damu, hakuna binadamu ambaye hawezi kuhitaji damu,” amesema Ahmed.