Ahmed awaomba mashabiki kununua tiketi za Jumapili mapema

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amewaomba mashabiki kununua tiketi mapema za mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex saa 10 jioni.

Ahmed amesema Uwanja wa Azam Complex ni mdogo hivyo ili kuepusha usumbufu Wanasimba wanapaswa kuhakikisha wananunua tiketi mapema.

Ahmed ameongeza kuwa tumeweka viingilio rafiki ili kuwawezesha Wanasimba kujitokeza kwa wingi na kuujaza uwanja mapema kusubiri siku ya Jumapili.

“Viingilio tumeweka rafiki lakini pia tukubaliane uwanja wa Azam Complex ni mdogo unaingiza 7,000. Mashabiki wanaotaka kuwepo uwanjani wanunue tiketi mapema ili kuepuka usumbufu,” amesema Ahmed.

Ahmed ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni Mzunguko ni Tsh. 10,000, VIP ni Tsh. 30,000 na Platinum ni Tsh. 150,000 ambayo utapata zawadi, usafiri, chakula ukiwa uwanjani.

“Watu wanasema Chamazi ni mbali lakini kwa watu wa Platinum haitakuwa hivyo sababu watakuwa wana usafiri maalum utakaosindikizwa na escort,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER