Ahmed awaita Wanambande Kwa Mkapa Ijumaa

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewaomba mashabiki wa maeneo ya Mbande, Kisewe na Chanika Mbondele kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly.
Ahmed anaendelea kuongoza idara ya hamasa kuelekea mchezo huo ambapo jana alianzia Magomeni Mikumi, Mbezi, Kibamba na Chuo cha Ardhi.
Ahmed amesema tuna nafasi kubwa ya kuitoa Al Ahly siku ya Ijumaa lakini itawezekana endapo tutakuwa kitu moja na mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.
Ahmed ameongeza kuwa hakuna namna Al Ahly watatoka salama katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kama mashabiki watajitokeza kwa wingi.
“Lengo letu kubwa lakuja hapa Mbande ni kuwatembelea na kuwaalika kwenye mechi yetu ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Ijumaa.”
Tunawahitaji Wanasimba wote katika dimba la Benjamin Mkapa ili twende kuipeleka Simba Nusu Fainali. Mechi hii inatuhitaji wana Simba wote tukaunganishe nguvu yovyote iwevyo tunahitaji nusu fainali.”
“Watu Mbande, Kisewe, Chanika Mbondele wote tunawahitaji kwa Mkapa siku ya Ijumaa,” amesema Ahmed Ally.
SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER