Ahmed aeleza hali ya kikosi nchini Guinea

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kikosi kimewasili salama nchini Guinea jana saa 11 jioni na kila kitu kinakwenda sawa kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya.

Ahmed amesema hali ya hewa ya Mji wa Conakry ambapo mchezo wetu utafanyika ni sawa na jijini Dar es Salaam hivyo wachezaji hawatapata changamoto yoyote inayohusiana na hali ya hewa.

Ahmed ameongeza kuwa kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho leo jioni katika uwanja wa (Stade General Lansana Conte)ambao utatumika kwenye mchezo wa kesho.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefika salama nchini Guinea jana jioni. Wachezaji walipewa mapumziko na watafanya mazoezi ya mwisho leo jioni kabla ya kesho kushuka uwanjani.

“Kwa kweli hatukupata changamoto yoyote ya nje ya uwanja, baada ya kufika usafiri ulikuwepo tayari kutupeleka hadi hotelini tulipofikia kwa hiyo hali ni nzuri,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER