Kiungo mkabaji, Abdallah Hamisi amejiunga na kikosi chetu kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru.
Abdallah anakuja kwenye kikosi chetu kuungana na Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Nassor Kapama na Fabrice Ngoma kwenye eneo hilo.
Abdallah ana uzoefu mkubwa na tunategemea atakuwa msaada kwenye kikosi sababu amecheza soka la kimataifa nje ya nchi kwa muda mrefu.
Abdallah amewahi kuzitumikia timu za
Muhoroni Youth FC, Sony Sugar, Bandari FC zote za nchini Kenya pamoja na Orapa United ya Botswana.
Malengo yetu ni kuhakikisha tunakuwa na wachezaji bora kwenye kila nafasi kwakuwa tunahitaji kufika mbali Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na kuchukua mataji ya ndani.