Kaimu Ofisa Habari wa klabu, Ally Shatry ‘Chico’ amesema maandalizi kuelekea mchezo wetu wa ligi kuu dhidi ya Yanga yanaendelea vizuri na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.
Chico amesema tunakumbuka tulipoteza kwa bao moja dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa msimu wa ligi 2021/22 na safari hii haitajitokeza tena ni zamu yetu kufurahia.
Chico ameongeza kuwa maandalizi ya mchezo yalianza tangu tukiwa Zambia na jana kikosi kimerejea nchini na moja kwa moja kimeingia kambini tayari kwa mchezo huo.
“Kikosi kimeingia kambini moja kwa moja kujiandaa baada ya kutoka Zambia kwa ajili ya mchezo huo. Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri morali ipo juu na kila mmoja anatamani kupata nafasi ya kucheza kuhakikisha tunapata ushindi.
“Walitufunga kwenye mechi ya Ngao ya Jamii lakini safari hii ni zamu yetu kuibuka na ushindi na hakuna kitakachotuzuia kutokana na maandalizi tunayoendelea kuyafanya,” amesema Chico.