Kikosi cha wachezaji 23 kimefika salama mkoani Mara tayari kwa mchezo wetu wa kwanza wa ligi dhidi ya Biashara United utakaopigwa kesho Jumanne katika Uwanja wa Karume saa 10 jioni.
Timu iliondoka jana saa 12 kwa Ndege kuelekea jijini Mwanza kabla ya leo asubuhi kuanza safari ya kuja Mara.
Kikosi hicho hicho ndicho kitaenda kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wetu wa pili utakaopigwa Septemba 30, katika Uwanja wa Jamhuri jijini humo.
Kikosi Kamili kinachosafiri
Makipa
- Ally Salim
- Beno Kakolanya
- Aishi Manula
Walinzi
- Israel Patrick
- Shomari Kapombe
- Mohamed Hussein
- Pascal Wawa
- Henock Inonga Baka
- Kennedy Juma
- Erasto Nyoni
Viungo
- Mzamiru Yassin
- Rally Bwalya
- Pape Sakho
- Peter Banda
- Hassan Dilunga
- Duncan Nyoni
- Taddeo Lwanga
- Jimmyson Mwinuke
Washambuliaji
- Chris Mugalu
- John Bocco
- Medie Kagere
- Yusuph Mhilu
- Kibu Denis