Kiungo wa Timu Taifa ya Zambia, Rainford Kalaba anatarajiwa kuwa sehemu ya wachezaji 23 wa TP Mazembe watakaokuja nchini Septemba 18 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Simba katika Tamasha la Simba Day Septemba 19, mwaka huu katika Uwanja Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Nyota huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji wakongwe wa timu hiyo atakuwa sehemu ya msafara huo ambao pia utakuwa na viongozi 12 na kufanya msafara huo kuwa na watu 35.
Simba imekuwa na mahusiano mazuri na timu hiyo kutoka Congo na mara kadhaa imekuwa ikicheza nayo michezo ya kirafiki. Mara ya mwisho kikosi hicho kuja nchini ni mwanzoni mwa mwaka huu ambapo ilikuja kushiriki mashindano ya Super Cup yaliyoandaliwa na Simba.
Kikosi Kamili
1. Mounkoro Ibrahim
2. Said Ngusia Baggio
3. Ochaya Joseph Benson
4. Atibu Radjabu Johnson
5. Issama Mpeko Djos
6. Masengo Yumba Godet
7. Tandi Mwape
8. Luzolo Nsita Ernest
9. Mundeko Zatu Kelvin
10. Kouame Koffi Cristian Raoul
11. Zemanga Soze Soze
12. Kalaba Rainford
13. Mayombo Etienne Raby
14. Sudi Bibonge Gondry
15. Mika Michee Michee
16. Bossu Nzali Adam
17. Kinzumbi Phillippes Beni
18. Ngimbi Vumbi Merceil
19. Bileko Mbaki Kelvin
20. Baleke Othos Jean
21. Beya Tumuteka Joel
22. Ntambwe Kalonji Magloire
23. Zola Kiaku Arsene