Bocco, Kagere kuongoza mashambulizi dhidi ya Gwambina leo, Morrison ndani

Nahodha John Bocco na kinara wa ufungaji Medie Kagere wataongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Gwambina FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Gwambina Complex uliopo Misungwi jijini Mwanza.

Mara kadhaa Kocha Didier Gomez amekuwa akitumia mshambuliaji mmoja na kuweka viungo watatu wa ushambuliaji lakini leo amekuja tofauti na kuwaanzisha Bocco na Kagere.

Hadi sasa Kagere ana mabao 11 na ndiye kinara wa ufungaji kwenye ligi  akifuatiwa na Bocco mwenye mabai 10.

Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison naye ameanza akichukua nafasi ya Luis Miquissone anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kikosi kamili kilivyopangwa

1. Aishi Manula

2. Shomari Kapombe

3. Mohamed Hussein

4. Kennedy Juma

5. Joash Onyango

6. Erasto Nyoni

7. Clatous Chama

8. Mzamiru Yassin

9. Medie Kagere

10. John Bocco ©

11. Bernard Morrison

Wachezaji wa Akiba

Gk.. Beno Kakolanya

02. Gadiel Michael

03. Ibrahim Ame

04. Jonas Mkude

05. Rally Bwalya

06. Chris Mugalu

07. Hassan Dilunga

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER