Mlinda mlango Aishi Manula, kiungo mshambuliaji Luis Miquissone na mlinzi Joash Onyango wameingia fainali ya tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi inayodhaminiwa na Emirate Aluminium Profile (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).
Kamati maalumu ya tuzo hizo, imepitisha wachezaji watano ambao wamefanya vizuri zaidi kwa mwezi husika na kuwachuja hadi kufikia watatu ambao wameingia fainali.
Wachezaji ambao waliingia tano bora ni Clatous Chama na Taddeo Lwanga pamoja na hao watatu waliongia fainali.
Mshindi wa tuzo hiyo atapatikana kupitia kura zitakazopigwa na mashabiki kupitia Website hii rasmi ya Klabu.
Tuzo hizo zilianza Februari ambapo Miquissone aliitwaa na kujishindia milioni moja kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium.
Zoezi la kupigiwa kura limeanza rasmi leo na litafungwa Machi 31, mwaka huu saa sita usiku ambapo utaratibu wa kuhesabu kura kisha kumtangaza mshindi utafanyika.
20 Responses
Ni wazo zuri kuwa na hizi tuzo zitazidi kuleta hamasa kwa wachezaji
Mungu utusimamie wanao tushinde mechi na As vita
Mungu ibariki simba Simba 🙏🙏
Nice web site
Tujipange vizuri kwa mchezo na Vita, hautakuwa mwepesi.
Tunahitaji ushindi katika mech ijayo mungu tupiganie
Na Mungu kwakuwa sio mwanadamu basi ameshatusikia maombi yetu na kayajibu sawasawa, sifa na utukufu ni vyake hata milele yote hakuna astahiliye zaidi yake.
Hallooo I’m number one Simba Sc die hard fan.
Hallooo
It is a good job
Napenda kuwapongeza wachezaji wote wa Simba sc ni wazuri
Mkenya na tena mwanasimba Kikamilifu🦁🦁
tusitolewe njiani na huo uvumi wa djuma shaban huenda wakawa wanataka kutufanyia mind game
Hows you guys
Jinsi ya kupiga kura
Tunapigaje kura kumchaguwa mchezaji Bora wa mwezi?
Nimefurahi kujumuishwa kwenye familia ya chama langu Pendwa duniani kwa sasa
Nimefurahi kujumuishwa kwenye familia yangu ya chama kubwa ya simba sport club
Aishi manula anastahili kuwa mshindi
Hongera Onyango our own…mwazo wali ku kejeli nani ka cheka leo.