Timu yafanya mazoezi ya mwisho Sokoine

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Uwanja wa Sokoine saa 10 jioni.

Mazoezi hayo ambayo yamesimamiwa na Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake yamefanyika katika Uwanja wa Sokoine ambao tutautumia kesho kwenye mchezo.

Wachezaji wote 22 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi ya kucheza kesho.

Ingawa tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunaiheshimu Tanzania Prisons lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua pointi tatu ugenini.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER