Kwaheri Valentin Nouma

Baada ya makubaliano ya pande mbili tumevunja mkataba na mlinzi wa kushoto Valentin Nouma raia wa Burkina Faso. Nouma tumemsajili kutoka St. Eloi Lupopo ya DR Congo msimu uliopita kwa mkataba wa miaka mitatu lakini sasa baada ya makubaliano haya hatakuwa sehemu ya kikosi chetu katika msimu wa mashindano 2025/2026. Katika kipindi cha mwaka mmoja […]

Asante Aishi Manula

Mlinda mlango, Aishi Manula hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu wa Ligi 2025/2026 baada ya kumaliza mkataba wake. Manula alijiunga nasi mwaka 2017 akitokea Azam FC na leo amehitimisha miaka nane ya kudumu kwenye kikosi chetu. Manula ameacha alama ndani ya klabu yetu ambapo alikuwa langoni kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa […]

Kwaheri Fabrice Ngoma

Ni rasmi kiungo mkabaji, Fabrice Ngoma hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa mashindano 2025/2026. Ngoma raia wa DR Congo alijiunga na kikosi chetu kutoka Al Hilal ya Sudan Julai mwaka 2023 kwa mkataba wa miaka miwili. Katika kipindi cha miaka miwili Ngoma amekuwa muhimili katika eneo la kiungo wa ulinzi wa timu […]

Omari Omari arejea Mashujaa kwa Mkopo

Kiungo mshambuliaji, Omari Omari amejiunga kwa mkopo na Mashujaa FC wa mwaka mmoja kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano 2025/2026. Omari alijiunga nasi msimu uliopita akitokea Mashujaa kwa mkataba wa miaka mitatu na sasa amerejea kwa mkopo kwa ‘Wanajeshi hao wa Mpakani’. Omari ni miongoni mwa wachezaji vijana wenye vipaji vikubwa ambao wanategemewa kujakuwa […]

Mo awataka Wanasimba kuwa watulivu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye ni Rais wa Klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amewataka mashabiki na wapenzi wa timu yetu kuwa watulivu kipindi hiki wakati tunapoandaa kikosi cha msimu ujao. Mo amesema mashabiki wanajisikia vibaya kutokana na jinsi tulivyomaliza msimu wa Ligi 2024/2025 lakini Uongozi unaendelea kuhakikisha tunakuwa na timu imara zaidi. Mo amesema huu […]

LATEST NEWS

FIXTURES

#NGUVUMOJA

Stay up to date with Simba Sports Club

THE CLUB
TEAMS
ACADEMY
FAN ZONE
SHOP

© 2022 Simba Sports Club | Website Administration by Kinara Technologies