Manula, Zimbwe, Banda, Mzamiru warejea kikosini

Nyota wetu sita waliokuwa kwenye timu za taifa wamerejea kikosini na moja kwa moja wamejiunga na wenzao kambini jijini Arusha.

Wachezaji hao ni mlinda mlango Aishi Manula, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin ambao walikuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars na Peter Banda aliyekuwa na timu yake ya Malawi ‘The Flames’.

Nyota hao wote wamewasili jijini hapa leo asubuhi na jioni wamefanya mazoezi pamoja na wenzao na kufanya kikosi chetu kukamilika.

Timu ipo Arusha kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kabla ya kurejea Dar es Salaam tayari kwa kilele cha Simba Day Septemba 19, mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER