Tumepoteza mbele ya Yanga Princess

Simba Queens imeshindwa kutinga fainali ya Ngao ya Jamii baada ya kupoteza kwa mikwaju ya penati 3-4 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Mchezo huo ambao ulikuwa mkali muda wote ulimalizika kwa sare ya kufungana bao moja katika dakika 90 za kawaida.

Yanga Princess walikuwa wa kwanza Agness kabla ya Jentrix Shikangwa kusawazisha dakika ya 90.

Katika mchezo huo penati zetu tatu zilifungwa na Precious Christopher, Jentrix na Asha Djafar.

Kwa upande wa waliopoteza mikwaju ya penati ni Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ na Vivian Corazone.

Baada ya kupoteza mchezo wa leo tutakutana na Ceasia Queens katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER