Fadlu: Tunahitaji Ushindi katika Mchezo wa Kesho

Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema pamoja nakuwa tumepata wiki tatu za maandalizi kuelekea msimu ujao wa ligi lakini tunahitaji kupata ushindi katika mchezo wa kesho wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

Kocha Fadlu amesema tumemsajili wachezaji wapya 14 kwenye kikosi chetu na wengi ni vijana huku wapinzani wetu wakiwa pamoja kwa muda mrefu lakini hilo halitusumbui na tupo tayari kwa ajili ya kupambana.

Aidha kocha Fadlu ameongeza kuwa kwenye kikosi chetu tuna aina tofauti za wachezaji kulingana na mpinzani tunayekutana naye kwahiyo tupo tayari kuikabili Yanga.

“Mchezo wa Kesho utatupa mwanga kuelekea msimu ujao wa Ligi, utatuonyesha maandalizi yetu ya wiki tatu kule Misri yalikuwa bora au la.

“Hatuna presha tutaingia kwenye mchezo wa kesho kama ilivyo kwenye mechi nyingine lakini tumejipanga kupata ushindi,” amesema Kocha Fadlu.

Kwa upande wake Nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na watafanyia kazi maagizo watajayopewa na walimu.

“Maandalizi yetu yamekamilika, sisi kama wachezaji tupo tayari kufuata maelekezo tutakayopewa na walimu wetu lakini lengo letu ni kushinda,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER