Kauli ya Mgunda kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Geita

Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex yamekamilika.

Mgunda amesema kikosi chake kimejipanga kucheza mechi ngumu kutoka kwa Geita lakini anaamini wachezaji watafuata maelekezo watakayowapatia.

Mgunda ameongeza kuwa wakati ligi ikiwa inaelekea ukingoni kila timu inakuwa imejipanga kuhakikisha inapata matokeo chanya na ndio maana nasi tupo tayari kumkabili kila aliye mbele yetu.

“Maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Geita yamekamilika, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na Ligi kuelekea ukingoni lakini tupo tayari kupambana ili kupata ushindi,” amesema Mgunda.

Mgunda ameongeza kuwa tutaingia katika mchezo wa kesho bila kuwadharau Geita kutokana na nafasi iliyopo badala yake tutacheza kwa malengo yale yale kutafuta pointi tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER