Tunamshukuru Rais Samia kwa zawadi ya ‘Bao la Mama’

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa milioni 30 za ‘bao la Mama’ kufuatia ushindi wa mabao 6-0 tuliopata dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Pesa hizo zimekabidhiwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro na kupokelewa na Try Again, Mwenyekiti wa Klabu Murtaza Mungungu na nahodha wa kikosi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Try Again amesema zawadai hii inatoa hamasa kwa wachezaji kupambana kwa ajili ya timu na mwisho wa siku mafanikio yanakuja kwa timu na Taifa kwa ujumla.

“Tunamshukuru Rais Samia kwa zawadi hii, baada ya kuipata hii tunaenda kujipanga kwa ajili ya robo fainali na mipango yetu ya kuvuka zaidi,” amesema Try Again.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mungungu amesema kikosi chetu kimeendelea kuimarika hivyo anaamini tutaendelea kupokea zawadi ya bao la mama.

Nae nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amempongeza Rais Samia kwa kutimiza ahadi hiyo huku pia akiwashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuisaidia timu kupata ushindi.

“Hii zawadi inazidi kutupa hamasa nasi tunaahidi hatutamuangusha. Vipi tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kutupa sapoti, tunawaomba muendelee kujitoa kwa ajili ya timu yenu,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER