Manula arejea langoni Kimataifa baada ya muda mrefu

Mlinda mlango Aishi Manula ameanza kwenye kikosi chetu kitakachoshuka dimbani kuikabili ASEC Mimosas usiku huu.

Mara ya mwisho Manula kucheza mechi ya kimataifa ilikuwa mchezo dhidi ya Horoya uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 18 mwaka jana na toka hapo hajacheza tena kutokana na kukumbwa na majeraha yaliomuweka nje ya uwanja kwa miezi mitano.

Kwa upande wake mlinzi Henock Inonga nae ameanza ikiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu arejee kikosini kutoka kwenye michuano ya AFCON.

Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Che Malone (20), Henock Inonga (29), Babacar Sarr (33), Saido Ntibazonkiza (10), Sadio Kanoute (8), Pa Omar Jobe (2), Fabrice Ngoma (6), Clatous Chama (17).

Ally Salim (1), David Kameta (3), Israel Mwenda (5), Kennedy Juma (26), Abdallah Hamisi (13), Mzamiru Yassin (19), Kibu Dennis (38), Luis Miquissone (11), Freddy Kouablan(18).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER