13 Wachukua fomu, wanne wautaka uenyekiti

Wagombea 13 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa klabu utakaofanyika Januari 29, mwakani.

Kati ya wagombea hao wanne wanawania nafasi ya mwenyekiti na tisa nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti ni aliyekuwa Mtunza Fedha wa klabu, Yusuph Nassor Majid ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS).

Wengine wanaowania ni Makamu Mwenyekiti wa zamaniĀ  Geofrey Nyange ‘Kaburu’ Yusuph Omar Yenga, na Eng. Rashid Khamsini.

Katika nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi mpaka sasa waliochukua fomu ni wagombea tisa.

Wagombea hao ni Iddy Noor Kajuna, Abubakar Zebo, Eng. Rashid Khamsini, Hawa Subira Mwaifunga, Laurian Mganga, Elisony Edward Mweladzi, Lameck Lawrance na Abdallah Rashid Mgomba.

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafungwa rasmi Disemba 19, mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER