Wiki ya Simba Kuzinduliwa Mafinga Agosti 31

Meneja Habari na Mawasiliano Ahmed Ally ametangaza tarehe rasmi ya uzinduzi wa wiki ya Simba ambayo itazinduliwa katika Viwanja vya Wambi wilaya ya mufindi Mafinga mjini mkoani Iringa, Agosti 31.

Ahmed amesema tumewahi kufanya uzinduzi wa wiki ya Simba sehemu mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma na mahali kwingine lakini hii ya Mafinga itakuwa ya tofauti kutokana na mpangilio wa matukio pamoja na burudani zitazokuwepo.

Ahmed amesema kutakuwa na msafara wa mabasi 10 aina ya Costa kutoka Dar es Salaam kuelekea Mafinga Agosti 30 na baada ya kufika kutakuwa na mkesha wa na asubuhi shughuli mbalimbali za kijamii zitafanyika kabla ya uzinduzi wenyewe kufanyika.

Ahmed ametaja matukio yote ambayo yatafanyika baada ya uzinduzi hadi kufika kilele chenyewe cha Simba Day, Septemba 10 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Septemba 2: Uchangiaji wa Damu kwa Wanasimba wote nchi nzima.

Septemba 3: Upangaji wa Droo kwa matawi yote yatakayo thibitisha kushiriki Simba Wiki Bonanza.

Septemba 4: Uzinduzi wa Matawi Mapya ya Simba ambayo yamekidhi vigezo.

Septemba 5: Biriani Day katika Kituo kitakacho pendekezwa cha Watoto Yatima.

Septemba 6: Siku ya Bonanza la Wiki ya Simba katika Viwanja vya Mwembe Yanga.

Septemba 7: Matembezi ya Hisani kuanzia Agha Khan kupitia Daraja la Tanzanite hadi Coco Beach.

Septemba 8: Benchi la Ufundi, wachezaji pamoja na viongozi kutoa msaada katika Kituo cha Watoto Yatima kitakacho pendekezwa.

Septemba 9: Mazoezi ya timu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na Mkutano wa Waandishi wa Habari kuelekea Simba Day.

Septemba 10: Kilele cha Simba Day katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER