Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mheshimiwa Simai Mohammed amepewa zawadi ya jezi ikiwa ni muendelezo wa kukutana na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya kutangaza Utalii.
Mheshimiwa Simai amekabidhiwa jezi hiyo na Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula akiwa na Meneja Habari na Mawasiliano Ahmed Ally huku akipewa jezi nyingine ampelekee Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ally Mwinyi.
Baada ya kukabidhiwa jezi hizo Mh. Simai ameushukuru Uongozi wa klabu kwa kujitolea kutangaza Utalii wa Zanzibar huku akiziomba klabu nyingine kufuata mfano wetu.
“Naupongeza Uongozi wa Simba kwa kazi kubwa mliyofanya wa kutangaza uchumi wa Zanzibar, tunaziomba timu nyingine kuiga mfano huu kwakuwa inaenda kuisaidia moja kwa moja pato la taifa,” amesema Mh. Simai.