Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa ametupongeza kuwa miongoni mwa klabu nane zitakazoshiriki michuano mipya ya African Football League (AFL) ambayo itaanza Oktoba 20.
Mh. Majaliwa ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma leo ambapo Simba inaitangaza nchi kimataifa na hilo ni jambo la kupongezwa.
“Mh. Spika nichukue nafasi hii kuipongeza klabu ya Simba kwakuwa moja ya timu nane bora barani Afrika ambayo itashiriki michuano ya African Football League.
“Hii ni heshima kubwa kwa Taifa ambayo Simba imeileta. Ufunguzi wa michuano hii itafanyika jijini Dar es Salaam Oktoba, 20 hivyo nawaomba mashabiki mjitokeze kwa wingi siku hiyo,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Katika mchezo huo wa ufunguzi utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa tutacheza na miamba ya Afrika, Al Ahly kutoka Misri.