Wawa: Hatutacheza kwa presha dhidi ya ASEC

Licha ya kuwaheshimu wapinzani wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, Asec Mimosas kutokana na kuwa bora lakini hatutaingia uwanjani tukiwa na presha kwenye mchezo wetu Jumapili.

Kauli hiyo imetolewa na mlinzi wa kati, Pascal Wawa ambaye ni raia wa Ivory Coast wanapotoka wapinzani wetu Asec.

Wawa amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora na aina ya uchezaji wa wapinzani lakini tunajiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda.

Wawa ameongeza kuwa wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na watahakikisha wanapambana ili kuhakikisha alama zote tatu zinabaki nyumbani.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Asec ni timu nzuri na ina historia kubwa Afrika lakini tumejipanga na hatutaingia uwanjani kwa presha wala woga.

“Tunafanya maandalizi kama tunavyojiandaa na mechi nyingine. Tunajua umuhimu wa mchezo na tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kubaki na alama tatu nyumbani,” amesema Wawa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER