Nyota wetu wanne wameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Nyota hao ni mlinda mlango, Aishi Manula kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin na washambuliaji John Bocco na Kibu Denis.
Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya nyama za paja Manula amerejea katika kikosi cha Stars.
Stars itacheza mechi mbili za kufuzu dhidi ya Niger na Morocco.