Walionunua tiketi za fainali ya Kombe Shirikisho kuzitumia Simba Day

Uongozi wa klabu umesema mashabiki 16,000 waliokuwa tayari wamenunua tiketi kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa sasa tiketi zao zitatumika katika Tamasha la Simba Day

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally Uwanja wa Amaan Zanzibar ambao utapigwa fainali hiyo unaingiza mashabiki 15,000 pekee hivyo tayari kuna watu 10,000 ambao wasingekuwa na nafasi hivyo tumeamua kuzitumia kwenye Simba Day.

Ahmed ameongeza baada ya kuthibitika mchezo utapigwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar tumesitisha zoezi la kuuza tiketi na waliokuwa wamenunua wanatakiwa kuzitunza hadi itakapofika Simba Day.

Aidha Ahmed amesema baada ya kufunga zoezi hilo sasa tiketi zitaanza kuuzwa upya kwa ajili ya fainali itakayopigwa Amaan Zanzibar.

“Uongozi ulikuwa unapambana kuhakikisha mchezo unapigwa Benjamin Mkapa lakini ilivyoshindikana imebidi tusitishe zoezi la kuuza tiketi huku walionunua wakiwa ni wengi zaidi ya uwezo wa uwanja wa Amaan Zanzibar,” amesema Ahmed.

Ahmed ametaja viingilio vya mchezo kuwa ni

VIP A Sh. 50,000
Jukwaa la Urusi 30,000
Mzunguko Sh. 10,000

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao.

Ahmed ameongeza kuwa kutakuwa na usafiri wa Ndege wa kwenda na kurudi siku ile ile ya mchezo ambayo gharama yake itakuwa Shilingi 350,000.

“Tutakuwa na usafiri wa Ndege wa kwenda na kurudi na mashabiki watakaolipa kiasi hicho watapata tiketi za VIP A, jezi za fainali pamoja na usafiri wa kutoka na kurudi Uwanja wa Ndege,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER