Meneja wa Habari na Mawalisiano wa klabu, Ahmed Ally amesema kikosi chetu kitaondoka leo saa mbili usiku kuelekea Morocco tayari kwa mchezo wa maruadiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Ijumaa.
Ahmed amesema msafara utagawanyika makundi mawili, Kundi la kwanza litaondoka leo na litakuwa watu na 29 wachezaji na benchi la ufundi wakati la pili litaondoka kesho likiwa na watu 20.
Tazama hadi mwisho kuona utaratibu wa safari utakavyokuwa kuanzia kuondoka na vituo itakavyopitia hadi kufika Morocco.