VIDEO: Simba Queens yakabidhiwa milioni 10 za Bao la Mama

Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa amekabidhi kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa Simba Queens ambazo ni ahadi ya hamasa kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan badaa ya kushiriki michuano ya CECAFA mwezi uliopita.

Msigwa ameitaka Queens kutokata tamaa kutokana na kushindwa kufikia malengo kutwaa ubingwa huku akiweka wazi kuwa sisi ndio timu bora nchini.

Awali wakati akimkaribisha kiongozi huyo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Bi Asha Baraka amesema Queens haitakata tamaa bali imejipanga kutetea ubingwa wetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER