Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Greyson Msigwa amewaambia wachezaji kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapongeza sana kwa kazi kubwa ya kupata ushindi dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia ugenini.
Msigwa ameyasema hayo wakati wa mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena alipokuwa akikabidhi Shilingi milioni tano kwa nahodha wa timu Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ikiwa ni zawadi ya ‘bao la mama’ kutokana na ushindi huo.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Msigwa amezungumzia pia tunachotakiwa kufanya katika mchezo unaofuata dhidi ya Bravos.