Meneja wa Kampuni ya uuzaji wa mafuta ya petroli, Diesel na Ndege ya Lake Energies, Muharami Mdemi amesema wamefurahi ushirikiano waliongia na klabu wa Simba Wese ambao ni kwa ajili ya Wanasimba nchi nzima.
Muharami amesema ushirikiano huo ni sehemu ya kurejesha kwa jamii ambapo watumiaji wa Simba Wese watakuwa wanapata pointi Kila wanapojaza mafuta Lake Energies na mwisho wa mwezi watakuwa wanapata zawadi mbalimbali.
Tazama video hii hadi mwisho Muharami amesema mipango yao ni kufanya ufunguzi mwingine katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Tanga.