Nyota wazamani na nahodha wa kikosi chetu, Abdallah Kibadeni amesema moja ya sababu iliyofanya kushindwa kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 1993 dhidi ya Stella Club ya Ivory Coast ilikuwa kujiamini kupita kiasi.
Kibadeni amesema tulitoka sare mchezo wa kwanza ugenini kwahiyo mechi ya marudiano nyumbani kila mtu aliamini tunaweza kushinda bila wasiwasi na tayari maandalizi ya kusherehekea ubingwa yalikuwa makubwa kuliko ya uwanjani kitu ambacho kilipelekea kushindwa kufikia malengo.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Kibadeni amefunguka mambo mengi ya zamani lakini pia amezungumzia mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya RS Berkane.