Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Al Masry yanaendelea vizuri na wachezaji wetu wapo kwenye hali nzuri tayari kuipigania timu.
Fadlu amesema baada ya kikosi kizima kuungana na kufanya mazoezi ya pamoja na kuzoea mazingira na hali ya hewa ya Misri anaamini tupo kwenye nafasi ya kufanya vizuri siku ya Jumatano.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Kocha Fadlu amezungumzia hali ya mlinda mlango Moussa Camara na kuhusu kama atakuwa sehemu ya mchezo au la.