Kocha Mkuu Fadlu Davids amewapongeza wachezaji kwa kiwango safi dhidi ya Coastal Union na kupelekea ushindi wa mabao matatu tukiwa hatujaruhusu bao.
Fadlu amesema ushindi wa leo utaongeza chachu kuelekea mchezo wetu wa ‘Dabi ya Karikaoo’ wikiendi ijayo na kuwafanya wachezaji kuwa katika hali ya kujiamini.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Kocha Fadlu amezungumzia pia viwango bora vilivyoonyeshwa na nyota wetu Steven Mukwala, Ally Salim na David Kameta ‘Duchu’.