Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema amefurahi kwa kufuzu Robo Fainali Shirikisho Afrika tukiwa na mchezo mkononi lakini ameweka wazi tulistahili kupata ushindi mnono dhidi ya Bravos Do Marquis.
Fadlu amesema tumepiga mashuti 26 langoni mwa Barvos na tumetengeneza nafasi nyingi ambazo zingeweza kutupa ushindi lakini haikuwa hivyo ingawa tulikuwa bora uwanjani kwenye kila kitu.
Tazama video hii hadi mwisho Kocha Fadlu amewapongeza benchi la ufundi, wachezaji na Idara ya utabibu kwa mafanikio haya.