Kaimu Mtendaji Mkuu wa Klabu, Zubeda Sakuru amewasisitiza Wanasimba wanaomiliki vyombo vya moto kujaza mafuta Lake Energies kwakuwa watakuwa wanasaidia kupatikana kwa mapato ya klabu.
CEO Zubeda ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Simba Wese ambao ni ushirikiano baina ya klabu na Lake Energies huku aliweka wazi mapato yanayopatikana yatasaidia kusajili wachezaji wakubwa.
Tazama video hii hadi mwisho nyota wetu Ladaki Chasambi na Elie Mpanzu wamewasilimu Wanasimba.