Kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua amesema anapoingia uwanjani jambo la kwanza ni kuisaidia timu kupata ushindi kufunga au kuasisti hilo jambo la ziada kwake.
Ahoua amesema anafahamu mwisho wa msimu kunakuwa na tuzo ya mchezaji bora (MVP) na kiungo bora ni jambo jema kuvipata lakini kwanza ni kuisaidia timu kufikia malengo yake ya kupata ubingwa.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahoua ameweka wazi matumaini yake kuiona Simba ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/25.