Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema kikosi kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga utakaopigwa Juni 15, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ahmed amesema wachezaji wote ambao hawapo kwenye majukumu ya timu za taifa ndio wamerejea mazoezini tayari kwa mchezo huo ambao utatupa tathimini kamili ya msimu mzima wa 2024/25.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahmed ametoa pia ratiba ya mechi zote zilizosalia.