VIDEO: Ahmed awatoa hofu Wanasimba kuhusu mechi ya pili ya Fainali ya Kombe la Shirikisho

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewatoa hofu Wanasimba kuhusu mechi yetu ya pili ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigwa Mei 25 kuwa taratibu zote kuhusu mchezo huo ziendelee kama zilivyopangwa.

Ahmed ametoa kauli hiyo kufuatia kuwepo taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kitu ambacho Ahmed amesema kwa sasa tunatakiwa kufikiria mchezo wetu wa Jumamosi.

Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahmed ameweka wazi kuwa baada ya mchezo wa Jumamosi ndio tutatangaza kuhusu mechi hiyo ya Mei 25.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER