Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amewaomba mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kesho katika Uwanja wa KMC Complex katika mchezo wa hatua ya 32 bora CRDB Federation Cup dhidi ya TMA Stars utakaoanza saa 10 jioni.
Ahmed amesema baada ya mashabiki kushindwa kuiona timu yao wikiendi iliyopita kesho ni siku yao la kupata burudani ambayo wameisubiri kwa muda.
Tazama mahojiano hadi mwisho Ahmed ameweka wazi kuwa hatutaidharau TMA na tutaingia uwanjani kwa tahadhari zote lengo likiwa kupata alama tatu na kutinga hatua inayofuata.