Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amesema licha ya kufanikiwa kufuzu kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini bado hatujamaliza kazi huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi Jumapili katika mchezo wa mwisho dhidi ya CS Constantine.
Ahmed amesema katika kundi letu ni Constantine ni pekee ambayo hatujaifunga na kwa ukubwa wetu Simba haitapendeza kupoteza mechi uwanja wa Benjamin Mkapa hivyo ni jukumu la kila Mwanasimba kuhakikisha anajitokeza ili kuipa sapoti timu.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahmed amesema safari hii atafanya hamasa ya Tawi kwa Tawi Dar es Salaam nzima.