Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema kuanzia sasa kiungo mshambuliaji, Elie Mpanzu ataitwa ‘Volcano’ kutokana na kasi aliyonayo hasa anaposhambulia lango la mpinzani.
Ahmed amesema mara zote Mpanzu anaposhika mpira wazo lake la kwanza ni kushambulia kwa kasi na hazuiliki na hilo ndilo lililomfanya kumbatiza jina la Volcano.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahmed amezungumzia pia viwango vya wachezaji vilivyoonyeshwa kwenye mchezo wa leo.