Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewasisitiza Wanachama wa Klabu wanaomiliki vyombo vya moto kuweka mafuta katika vituo vya Lake Energies kwakuwa kila lita moja wanayojaza klabu inapata asilimia ya mapato.
Ahmed amesema kwenye vituo vyote vya Lake Energies ukijaza mafuta kwa njia ya mtandao (simu za mkononi na Sim Banking) ambayo itakuwa inasaidia Moja kwa Moja klabu.
Tazama video hii hadi mwisho Ahmed ametaja sababu ya klabu kuingia makubaliano na Lake Energies na sio Kampuni nyingine.