Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone hajaumia popote kwenye ajali aliyopata usiku wa kuamkia leo eneo la Mikocheni, Dar es Salaam.
Ahmed amesema, Che Malone alikuwa ameenda kuwapokea ndugu zake Uwanja wa Ndege kutoka Cameroon saa 10 alfajiri na alipokuwa anaendesha gari wakati wa kurudi ndipo alipopata ajali hiyo.
Tazama mahojiano haya mpaka mwisho kujua kilichotokea na hali ya mchezaji na majeruhi ilivyo baada ya vipimo vya madaktari.